TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI POSTA 2024

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI POSTA 2024

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji wote wanafasi mbalimbali za kazi kufika kwa ajili ya usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15/06/2024 hadi 21/06/2024 hatimaye kuajiriwa waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ya tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada;
2. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka;
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of
results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
7. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
9. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi;
10. Wasailiwa wote mnaelekezwa kufika eneo la usaili dakika arobaini (40) kabla ya muda wa Usaili uliopangwa kuanza; na
11. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

DOWNLOAD PDF HAPA CHINI

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*